Jinsi Ya Kupika Viazi na Nyama ya Kuku na Ng'ombe ZilizochomwaMimi ni mpishi ambaye zaidi nimebobea kwenye kuchoma nyama. Hivyo kupitia nyama za kuchoma nimevumbua kuwa nyama zilizochomwa ukizitumia katika mapishi mengine inaleta ladha nzuri zaidi. Leo nakuelekeza hapa jinsi waweza pika kwa kutumia viazi. tena waweza tumia ndizi kama sio viazi.

Nyama Zilizochomwa weza choma mwenywe au ukanunua ambazo zimechomwa tayari kutoka kwangu .... kama ukija kula nyama.

MAHITAJI mlo wa watu 3


 • Kuku Choma 1/2 - kata vipande vipande
 • Ng'ombe Choma 1/4 - kata vipande vipande
 • Viazi 1/2 kg - menya 
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Mafuta ya Kula Vijiko 2 vya mezani
 • Binzari njano - 1/4 kijiko cha chai
 • Bay Leaves - Majani mawili 
 • Mixed Hearbs - 1/2 kijiko cha chai
 • Pilipili - kama wapenda 
 • Kitunguu swaumu punje 4 - twanga
 • kitunguu maji 2 - katakata
 • Maji kwa kupikia

JINSI YA KUPIKA 1. Weka kila kitu katika sufuria moja, anza na viazi, kisha nyama na malizia na viungi vyote na mafuta. Kisha weka majihadi yakaribie viazi. Weka moto wa kati na wacha vichemke kwa dakika 15-20  au mpaka pale utakapoona viazi vimeiva. 
 2. Ikiwa katika kupika maji yatapungua unaweza kuongeza. 
 3. Kufanya pishi lilonona zaidi waweza kutumia butter badala ya mafuta ya kawaida. No comments:

Post a Comment

@chefkile