Jinsi ya Kutengeneza Salad ya Mchanganyiko wa Matunda na KabichiMatunda ni matamu sana kama yalivyo ila pia ukiyachanganya unapata kitu kitamu zaidi. Sasa katika mchanganyiko huu wa matunda kabechi inahusika kama ifuatavyo.

Matunda mix kwa watu 2

 MAHITAJI 


  • Embe dodo 1 ( Menya na kulikata kata vipande vidogo vidogo) 
  • Karoti 2 ( kwangu ganda la juu na kukata kata vipande vidogo vidogo) 
  • Kabechi 1/4 (Kata ndogo ndogo kisha loweka kwa maji moto kwa dakika 2 ) 
  • Tango 1 ( menya na kulikataka kata ila ondoa mbegu za ndani) 
  • Maji ya limao vijiko vya 2 vya mezani 
  • Parachichi 1 ( menya na kulikata kata) 
  • Chumvi kidogo tu - au lah kwa kiasi upendacho 

 NAMNA YA KUCHANGANYA   1. Ni rahisi sana changanya vyote katika bakuli au chombo kitoshacho. Na hapo ni tayari kwa kula. Ni mchanyanyiko mtamu sana 
 *MUHIMU* • Embe liwe limeiva vizuri • Parachichi liwe limeiva vizuri

No comments:

Post a Comment

@chefkile