Jinsi ya Kupika Supu ya KukuHili ni moja ya mapishi marahisi kabisa. Naita supu ila waweza ita mchemsho au waweza ifanya mchuzi kabisa kwa kulia wali au chapati.

Mlo wa watu 2

MAHITAJI


  • Kuku nusu - katakata vipande vidogo vidogo
  • Kitunguu Swaumu punje mbili - twanga
  • Juisi ya Chungwa moja
  • Pilipili Manga nusu kijiko cha chai 
  • Udaha ( cayenne Spices) robo kijiko cha chai
  • Chumvi Kiasi utakacho
  • Dry Oregano - nusu kijiko cha chai

JINSI YA KUPIKA  1. Weka kuku katika chungu chako na na maji nusu lita, weka viungo vingine vyote ispokuwa juisi ya chungwa. Wacha ichemke kabisa. 
  2. Ikiisha kuiva kabisa, kamulia ile juisi ya chungwa kisha acha vichemke pamoja kwa dakika 3. Baada ya hapo ni tayari kwa matumizi. 

No comments:

Post a Comment

@chefkile