Jinsi Ya kupika Supu ya Kuku Baada ya KumchomaKuna mapishi mengi sana ya supu ila leo hapa nakuonyesha jinsi ya kuandaa supu ya kuku kwa kutumia kuku ilokwisha kuchomwa.  Supu hii huwa haichelewi sana maana nyama huwa imeiva yatari. Ni raha sana kama ikiwa utaopata kuku ambayo ilichomwa na mkaa, au kuni ili kupata ladha ya moshi moshi .

Supu ya Watu wawili

MAHITAJI

 • Vipande viinne ya kuku - ( ilokwisha chomwa ikapoa)
 • Vitunguu maji 2 ( kata pande kubwa kubwa)
 • Kitunguu swaumu Punje 2 (Twanga)
 • Chumvi Kiasi upendacho
 • Pilipili Manga 1/4 kijiko cha chai
 • Mafuta ya Kula 1 kijiko cha mezani
 • Karoti 1 - Kata vipande vipande
 • Pili Pili Hoho  - Moja kata upendavyo
 • Pilipili Kiasi upendacho (Sio lazima)


JINSI YA KUPIKA

 1. Katika chombo unachotaka kutumia kupika. weka vitu vyote kwanza kama vitunguu, hoho, karoti na viungi vingine. kisha weka vipande vya kuku. Ongeza maji hadi kukaribia kufunika kuku ila yasifunike. Funika na weka joto la kati
 2. Chemsha kwa dakika kumi. Baada ya hapo ni tayari kwa kula. 

No comments:

Post a Comment

@chefkile