Jinsi ya Kupika Miguu ya Kuku na NdiziAwali nilionyesha namna ya kukaanga miguu ya kuku na ile sauce yake, hapa nitakuonyesha jinsi ya kuandaa mchemsho mzuri kwa kutumia miguu ya kuku na ndizi mzuzu ingawa unaweza kutumia hata ndizo aina ingine maana hatua ni zile zile.

 Mchemsho kwa watu 2

 MAHITAJI


 • Ndizi mzuzu 6
 • Miguu 6 ya kuku
 • Karoti 1 ( kwangua na kuishafisha vema) 
 • kitunguu kimoja ( menya katakata) 
 • Chumvi kiasi kidogo 
 • Viungo mchanganyiko vya mimea ( mixed herbs) kijiko 1 cha mezani
 • Mafuta ya kupikia kijiko kimoja cha mezani ( olive oil au mafuta yoyote mazuri ya mimea) 

NAMNA YA KUPIKA

 1. Kwanza anza na kumenya ndizi zako na kuzichemsha - Katika kuzichemsha weka , chumvi, mafuta na maji kiasi - Chemsha kwa dakika 3 ha 5 
 2. Ikiisha kuchemka kwa muda huo ndipo uweke ile miguu ya kuku pamoja na mixed herbs, vitunguu na karoti. Ikiwa inahitaji uongeze maji basi ongeza kisha chemsha tena kwa dakika 10 had 15 
 3. Maji yasikauke maana lengo supu ipatikane. 
 4. Baada ya hapo mchemsho huo mtamu uko tayari kwa kuliwa. Bila shaka umefurahia huo mchemsho

No comments:

Post a Comment

@chefkile