Jinsi ya Kupika Mboga ya Mnafu na KarangaLeo kwa uzuri kabisa naonyesha namna ya kupika mboga ya mnafu kwa karanga. Nakwambia mara tu utakapoliwezea hili pishi. Utakuwa unakula mara kwa mara. 

MAHITAJI 


  • Mnafu fungu moja ( chambua na kuikatakata) 
  • Punje mbili za Garlic - chopped 
  • Kitunguu Maji - chopped 
  • Peanut Butter vijiko 2 
  • Chumvi kama upendavyo
  • Pilipili Kama unapenda 

JINSI YA KUPIKA   1. Anza kwaa kuunga kitunguu maji na garlic kwa dakika chache Kisha weka maji kidogo yakianza kuchemka weka Peanut butter - Endelea kukoroga hadi ilainike na kuwa nzuri katika uzito uupendao - mimi napenda nzito kidogo - Unaweza kubalance uzito wa butter cream kwa maji
  2. Ikifikia poa ndipo unaweka ile mboga yako na kuvichanganya vizuri kama inakuwa nzito sana ongeza maji kidogo - Weka pilipili kama unapenda Sasa ni mda gani itachemka hapo ni juu ya mpishi vile unapendelea kupika mboga yako. Binafsi huwa nazima kabisa jiko na kuivisha mboga majani na joto tu kwa dakika chache kisha nakula.

No comments:

Post a Comment

@chefkile