Jinsi ya Kupika Maharage na Kuunga kwa NaziMaharage ni moja ya mboga inayoliwa sana hapa kwetu Tanzania. Mimi personally napenda sana maharage hasa yakiungwa na nazi ikakolea vizuri. Katika hali ya kawaida unaweza ukachemsha maharage yakaiva, ukaweka chumvi kidogo na kitunguu... vikachemka tena kidogo. Yakawa tayari kwa kula. Ila sikuhizi vikolombwezo kibao.... kama navyokuonyesha hapa jinsi niliyaunga maharage haya.

MAHITAJI


 • Maharage 1/4 kg
 • Tui la Nazi moja zito
 • Vitunguu maji 1 - katakata
 • Mchanganyiko wa Kitunguu swaumu na tangawizi - Kijiko cha mezani kimoja
 • Chumvi Kiasi upendacho
 • Binzari manjano - 1/4 kijiko cha chai - just for some color
 • Pilipili manga 1/4 kijiko cha chai
 • Pilipili (sio lazima)

JINSI YA KUPIKA 


 1. Kwanza kabisa chemsha maharage hadi yaive kabisa
 2. Weka viungo vingine vyote isipikuwa nazi. kisha wacha vichemke zaidi kwa dakika 7-10 . ikiwa maji yamepungua waweza kuongeza kidogo tu.
 3. Sasa weka tui la nazi na uendelee kukoroga kwa dakika 3 hivi yaani hadi machanganyiko utakapoanza kuchemka tena. Kukoroga kunasaidia tui kutokukauka. 
 4. Baada ya hapo ni tayari kwa kula kwa wali, ugali au chapati.

No comments:

Post a Comment

@chefkile