Jinsi ya Kupika Chapati ya Unga wa DonaChapati hii ya unga wa mahindi niliijua nilipokuwa na umri kama miaka 10 hivi, nilipokuwa naishi jijini Dar es Salaam kwa mlezi wangu. Alikuwa mfugaji wa kuku wa mayai. Sasa sisi tukiwa ndio watoto tulikuwa tunafanya shughuli za kusaidia na ufugaji wa kuku hivyo mayai tuliyala sana. Sasa kwa vile tulikuwa tunakula kila siku tukawa tunatafuta namna ya kufanya yawe tofauti ndipo siku moja tukachanganya na unda wa mahindi enzi hizo ni sembe ila hivi nimekuwa nachanganya na dona. Nawe unaweza maana ni rahisi sana kama nilivyoelezea hapa.

Kwa Chapati 2

MAHITAJI 


  • Unga wa dona vijiko 3 vya chakula 
  • Sukari vijiko 3 vya chai
  • Mayai 3 
  • Mafuta ya kupikia ile kawaida kama wapika chapati 
  • Siagi ya Karanga 

JINSI YA KUANDAA   1. Weka unga katika chombo, pasua mayai yote, weka sukari kisha koroga hadi iwe laini kabisa. Kama ikiwa haiwi laini ongeza yai moja ila sio maji.
  2. Weka chombo cha kupikia katika moto na mafuta kidogo; yakiisha kupata moto weka ule mchanganyiko kwa kipimo cha macho kuona hii ni chapati moja... Ivisha upande mmoja kwa dakika 2 kisha igeuze fanya kama mara mbili tatu. Na hapo itakuwa tayari na endelea kwa chapati ingine ivo. Baada ya hapo chapati zipo tayari ; waweza zipaka ile siagi ya karanga au jam kwa vile upendavyo. Katika pishi hili kuna vitu vichache ila kama ujuavyo mapishi ni sanaa waweza ongeza vibwagizo vingine vingine.

No comments:

Post a Comment

@chefkile