Jinsi ya Kuchoma Kidari cha KukuHiki ni mojawapo ya vyakula naona viko na afya sana ( healthy meal). Kinahusisha kuchoma kuku na mahidi ya kuchemsha pamoja na mboga za majani.

Kwa mlo wa watu 2

MAHITAJI 


  • Vidali vya kuku viwili 
  • Masala ya kuchoma kuku ( chicken masala) zipo aina nyingi ila tandori nzuri zaidi 
  • Hindi moja bichi - Pukuchua na kulichemsha hadi kuiva kabisa 
  • Spinach - Mafungu mawili - Yaoshwe na kukatwa katwa 
  • Kitunguu maji kimoja 
  • Mafuta ya kula ya olive oil au yoyote ya mimea 
  • Chumvi kijiko kimoja cha chakula - nusu kwa kuku na nusu kwa mboga 

JINSI YA KUANDAA MLO HUU   1. Kwanza chukua vidali vya kuku na kuvipakaa masala, chumvi na mafuta kidogo kisha acha viungo viingie kwa dakika 15 hadi 20. Andaa jiko la kuchomea wakati vidali vinapata viungo kunoga ( marinating process) 
  2. Jiko likiwa tayari na na dakika za marinating tayari ni muda wa kuchoma kuku yako - itatatemea kama ni oven au grill - ila choma upande mmoja kwa dakika 10 hadi 15 na vinyo hivyo upande mwingine kisha weka pembeni na ifunike na jito lake. 
  3. Sasa andaa mboga yako - weka chombo na mafuta kidogo kisha weka vitunguu maji na ivisha kwa dakika chache na uweke mboga ya spinach ivisha kidogo ndipo uweke mahindi yale yaliochemshwa. Mimi katika mboga nimeweka vitu vichache ila unaweza weka nakshi zaidi kwa kuongeza vitu zaidi kama, karoti, hoho, tui la nazi, kabichi n.k Baada ya mboga kuiva kwa dakika takribaki 8 hivi ipo tayari kwa kuliwa , pakuwa mboga na uweke kipande cha kidari na ufurahie mlo wako.

No comments:

Post a Comment

@chefkile