Jinsi ya Kuandaa Mishikaki ya Maini na Figo Ya Ng'ombe


Maini na figo ni nyama za ndani za Ng'ombe. Huwa nikizipata napendelea kuroast au kutengeneza mishikaki. Hapa nakuonyesha viungo nilivyotumia kufanya marination.

MHITAJI


 • Maini na Figo - 1/4kg  ( Katakata vipande vidogo)
 • Pilipili Manga - Nusu kijiko cha chai
 • Udaha ( cayenne) robo kijiko cha chai
 • Punje 3 za kitunguu swaumu - twanga
 • Tangawizi Paste - kijiko kimoja cha chai
 • Soy Sauce - Jiko kimoja cha chai
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Mafuta ya Kula kijiko kimoja cha mezani
 • Stiki za Mishikaki ( Ziloeke kwenye maji kwa dakika 30) Itazuia kushika moto kwa haraka

 JINSI YA KUANDAA


 1. Chukua bakuli weka maini na figo kisha weka na viungo vyote. Ukiisha changanya vema wacha vikae kwa dakika 20.
 2. Baada ya dakika 20 anda kuweka mishikaki yako katika vijiti. Kisha anza kuchoma kwa moto usio mkali sana.
 3. Ikiisha iva... waweza tengeneza chachandu yako ukala au ukakamulia limao tu ukala.

No comments:

Post a Comment

@chefkile